Mkuu wa jeshi aponea kifo Somalia

Image caption Jenerali Dahir anaendesha moja ya magari yenye uwezo mkubwa wa kudhibiti mashambulizi

Mkuu wa jeshi la Somalia ameponea chupuchupu kuuawa mjini Mogadishu.

Hili ndilo shambulio la punde zaidi katika msururu wa mashambulio dhidi ya viongozi wa serikali na rasilimali za serikali nchini humo.

Gari lake Jenerali Dahir Aden Elmim lilirushiwa bomu katika barabara kuu karibu na afisi za wizara ya ulinzi mjini Mogadishu.

Aliponea kwa sababu yeye huendesha mojawepo ya magari machache yaliyo na uwezo wa kudhibiti shambulio la risasi, ambayo yametengewa viongozi wakuu wa serikali hiyo.

Hakuna yeyote aliyedai kuhusika na shambulio hilo kufikia sasa japo inafahamika kuwa kundi la Al shabaab limekuwa likifanya mashambulio ya mara kwa mara mjini Mogadishu.

Mwishoni mwa juma, watu 15 waliuawa katika shambulio lililolenga jengo la bunge la Somalia. Wengine wengi walijeruhiwa wakiwemo wabunge 3.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii