Manchester United ni mayatima

Image caption Mmiliki wa Man united ameaga dunia

Mmiliki wa Manchester United mmarekani Malcom Glazer ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 85 .

Familia ya bwenyenye huyo ilinunua United kwa gharama ya Euro milioni 790 mnamo mwezi Mei mwaka wa 2005 licha ya pingamizi kali kutoka a kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Hata hivyo, Chini ya umiliki wake uliosabibisha deni kubwa kwa klabu hiyo ''the Red Devils'' walishinda taji la premia ya Uingereza mara tano na vile vile taji la klabu bingwa mwaka wa 2008 .

Wanawe mmarekani huyo waliozaliwa Marekani Byan, Joel, na Avram wote wamejumuishwa katika bodi ya klabu hiyo, huku Joel na Avram wakiwa wenyekiti wenza.

Kifo cha Glazer hakitarajiwi kuadhiri umiliki wa United, kwani familia hiyo bado inamiliki asilimia 90 za hisa za klabu hiyo .

Asilimia 10 inayosalia inamilikiwa na wenyehisa katika soko la hisa la NY stock Exchange.

Image caption Mmiliki wa Man united ameaga dunia

Glazer alikuwa pia mmiliki wa Tampa Bay Buccaneers, iliyobadili sura ya kandanda ya Marekani kwa kushinda taji la Super Bowl .

Bwenyenye huyo ambaye hakuwahi kanyaga uwanjani Old Trafford kutokana na hofu ya kuwaudhi mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa wanamsuta kwa kupanga njama ya kuinunua klabu hiyo kwa kutumia madeni.

Glazer inasemekana alianza kisiriri kuwashawishi wenye hisa wa klabu hicho kumuuzia hisa zao tangu mwaka wa 2003 kabla ya kutwaa umiliki wama wa 2005.

United ambayo msimu uliopita ilitangaza faida kubwa ya asilimia 20 yaani pauni milioni 418 inakabiliwa na deni la zaidi ya pauni milioni 400.

Glazer aliyeugua kiharusi tangu mwaka wa 2006 amewawachia wanawe sita umiliki wa klabu hiyo ya Uingereza.