Makasisi waliotekwa nyara waachiliwa.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kituo cha uhamiaji kati ya mpaka wa Cameroon na Nigeria

Makasisi wawili kutoka nchini Italy pamoja na mwanamke mmoja raia wa Canada waliotekwanyara na kundi la Boko Haram nchini Cameroon wameachiliwa huru.

Idara ya mawasiliano nchini Cameroon imesema watatu hao wako katika afya nzuri na wameabiri ndege inayoelekea katika mji mkuu wa Younde.

Walipelekwa kazkazini mwa taifa hilo karibu na mpaka na Nigeria.

Majina ya makasisi hao ni Giampaolo Martana na Giantonio Allegri.