Ni Rasmi sasa Al Sisi ndiye Rais - Misri

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption AL SIsi ashinda uchaguzi

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa urais nchini Misri yamethibitisha kuwa Abdul Fattah AL Sisi ameshinda urais.

Matokeo hayo yameonesha kuwa AL Sisi, ambae alikuwa mkuu wa jeshi, amepata kura nyingi zaidi.

Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa AL Sisi amepta asili mia 96.6 ya kura zote zilizopigwa akiwa amempiku mpizanani wake mkuu ambaye alipata chini ya asili mia 3 pekee.

Inakisiwa kuwa chini ya nusu ya watu wote waliojiandikisha kupiga kura walijitokeza kupiga kura.

Bwana Sisi, alipata umaarufu mkubwa mwaka uliopita baada ya kumpindua rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia, kiongozi wa kiislamu Mohammed Morsi.

Bwana Sisi pia alipiga marufuku vuguvugu la Muslim Brotherhood la Mohammed Morsi.

Katika hotuba yake ya kwanza, rais huyo mpya wa Misri amewaahidi raia kuwarejeshea matumaini na kuwapa maisha bora katika siku zijazo.