Hofu ya mfumuko wa bei Ulaya

Haki miliki ya picha af
Image caption Kuna hofu kwamba mfumuko wa bei huenda ukatikisa tena bara Ulaya

Banki Kuu ya Muungano wa Ulaya inatarajiwa kuchukua hatua kadhaa Alhamisi, kushughulikia hofu kuwa mataifa wanachama wa Ulaya huenda yakakabiliwa na mfumuko wa bei.

Uchumi katika maeneo ya Jumuiya ya Ulaya yanaendelea kukua lakini kwa mwendo wa kobe sana na kukosa kuongezeka kwa bei za bidhaa kumetajwa kama sababu mojawapo inayozuia kufufuka kwa uchumi.

Kuongezeka kwa bei za bidhaa barani Ulaya kumekua kwa kiwango cha chini mno, takwimu zikionesha kuwa bei ya bidhaa iliimarika kwa asilimia 0.5.

Iwapo bei za bidhaa nchini humo zitaporomoka zaidi, kuna uwezekano mkubwa kuwa wanunuzi watachelea kulipia bidhaa zao wakisubiri bei ishuke zaidi ili wanufaike kwa faida ya juu.

Kushuka kwa bei za bidhaa pia kunaweza kuvuruga mipango ya kulipa madeni.

Benki Kuu ya Jumuiya ya Ulaya inatazamia kuyaepusha mataifa shirika na tatizo hilo la kiuchumi kwa kupunguza kiwango cha riba inachotoza.

Benki hiyo pia, inatazamia kupunguza faida inayopatikana kwa wale wanaoweka pesa zao kwa akiba hivi kwamba, watanufaika zaidi iwapo watawakopesha wawekezaji mtaaji wa biashara .

Aidha benki hiyo inapania kutekeleza sera hizo miongoni mwa zingine madhubuti kuhakikisha kuwa mikopo ya mtaaji ni nafuu zaidi kwa wawekezaji .