Maandamano zaidi Brazil

Haki miliki ya picha b
Image caption Maelfu waandamana kupinga kombe la dunia

Maelfu ya wenyeji wasio na makao mjini Sao Paolo waliandamana nje ya uwanja utakaoandaa mechi ya kwanza ya kombe la dunia alhamisi ijayo wakipinga gharama ya juu ya mashindano hayo.

Maandamano hayo yaliwadia siku moja tu baada ya rais wa Brazil Dilma Rousseff kuwahakikishia wageni na mashabiki wa kandanda kuwa kamwe hatoruhusu maandamano yatie doa kwenye kipute hicho cha kombe la dunia.

Image caption Maelfu waandamana kupinga kombe la dunia

Takriban waandamanaji 10,000 waliziba barabara zote mjini Sao Paolo wakiishinikiza serikali ya bi Rousseff iwekeze katika sekta ya afya elimu na ipunguze gharama ya juu ya usafiri wa umma.

Zaidi ya watu milioni moja waliandamana katika barabara za miji yote ya Brazil wakishinikiza serikali kupunguza ubadhirifu wa fedha na kupunguza matumizi yake kwa maandalizi ya kombe la dunia na yale ya Olimpiki yatakayofanyika mjini Rio mwaka wa 2016.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption 10,000 Waandamana kupinga Kombe la Dunia

Licha ya hakikisho la rais Rousseff wafanyikazi wa reli walitishia kuanza mgomo upya huku polisi wa trafiki mjini Sao Paolo pia wakitishia kuanza mgomo Alhamisi.

Mapema wiki hii serikali iliwaongezea polisi wote mshahara ilikuzuia mgomo uliotishia kuporomosha hali ya utengamano huku fainali ya kombe la dunia likinukia.

Serikali imeahidi kutumia polisi na hata jeshi la taifa kudumisha amani na utengamano wakati wa kombe la dunia.