Emir wa Kano,Nigeria hatimaye azikwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Emir wa Kano Al hajj Ado Bayero

Mazishi ya Emir wa eneo la KANO kazkazini mwa Nigeria yamefanyika.

Al haji Ado Bayero mmoja wa viongozi wa kidini anayeheshimiwa sana nchini humo alifariki mapema siku ya ijumaa akiwa na umri wa miaka 83.

Ni kiongozi wa pili kwa ukubwa wa dini ya kiislamu baada ya Sultan wa Sokoto.

Mwili wake ulizikwa katika makaburi ambayo mababu zake walizikwa karibu na nyumba yake huko Kano.

Kiongozi huyo wa dini alikuwa mkosoaji mkubwa wa kundi la wanamgambo wa boko haram.

Alinusurika shambulizi la mauaji na washukiwa wa kundi hilo mwaka uliopita.