Uzazi, elimu au kazi?

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Mwanamke anaweza kupoteza uwezo wa kuzaa kuanzia umri wa miaka 35

Mtangazaji mmoja mwanamke anawashauri wanawake kuweka mipango yao ya elimu ya juu na kazi kando ili kuweza kupata watoto kwa sababu uwezo wa mwanamke kuzaa hupungua na umri.

Katika mahojiano na mtangazaji maarufu wa BBC, Jeremy Paxman, mwanamke huyo Bi Allsopp, alisema kuwa,'' wanawake pia wanapaswa kuwa wakweli kuhusu umri wao akisema kwamba swala hilo bado ni mwiko miongoni mwa wanawake.

Sasa je nini ukweli kuhusu umri unaofaa kwa wanawake kupata watoto?

Kwa mujibu wa takwimu zilizochapishwa mwaka 2013 nchini Uingereza, wanawake bila shaka hawapaswi kupoteza matumai ikiwa umepita umri wa kuzaa yaani kati ya miaka 25-40

'Umri upi unafaa?'

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kirstie Allsopp anahoji ikiwa mwanamke anapaswa kuweka swala la elimu ya juu kando na kupata familia

Kwa mujibu wa utafiti huo, asilimia 80 ya wazazi wataweza kupata mtoto chini ya mwaka mmoja ikiwa mwanamke ana umri wa miaka 40. Sharti ni kwamba wawe wanajihusisha na tendo la ndoa karibu kila siku na wala wasitumie mpango wa uzazi.

Utafiti huo unasema kuwa wale ambao hawapati watoto katika mwaka wa kwanza, takriban nusu yao watajifungua katika mwaka wao wa pili wa ndoa.

Idadi ya wanawake ambao wanapatwa na shida ya kushika mimba ni asilimia kumi nchini Uingereza. Bi Allsopp, anahoji ikiwa ni sawa kwa wanawake kuweka kando mpango wa elimu ya juu zaidi ili kupatia kipaombele swala la uzazi? Nini maoni yako?

Tunajua vyema kuwa uwezo wa mwanamke kushika mimba hupungua kadri umri wake unapoendelea kukua.

Lakini wataalamu wanasema kwamba sio rahisi kama inavyodhaniwa.

Wanawake wengine wanapata ugumu kushika mimba hata wakiwa na umri wa miaka 20 kuelekea juu wakati wengine wakigundua kuwa hawana tatizo la kuzaa hata wakiwa na zaidi ya miaka 40.

'Mfumo wa maisha'

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Kupata kazi nzuri huwa ni kikwazo katika swala la kupata watoto

Licha ya kujihusisha na tendo la ndoa kila siku, kuna baadhi ya watu ambao hawawezi kushika mimba, sababu za tatizo hilo ni nyingi

Mfumo wa maisha ukiwa moja ya sababu hizo, lakini wakati mwingi huwa ni vigumu kueleza kwa nini mwanamke hawezi kushika mimba.

Watoto wasichana huzaliwa wakiwa na mayai mengi, karibu milioni moja. Lakini wanapovunja ungo huwa ni mayai 400,000 pekee ambayo huwa yamebakia mwilini.

Mayai haya huendelea kupungua mwanamke anapokuwa. Takriban mayai 1,000 hupotea kila mwazi.

Wataalamu wa afya wanasema ni bora kwa wanawake kujaribu kupata watoto wanapokuwa wachanga wa umri kuanzia miaka 20 hadi thelathini na tano. Ujauzito wao hautakuwa na changamoto nyingi na pia itakuwa rahisi kwao kujifungua na pia kufurahia watoto wao.

Lakini mfumo wa siku hizi wa maisha hauwezi kuruhusu hilo kufanyika.

Elimu ya juu, kazi na kumsaka 'Mr Right' au mwanamume unayemuona kuwa sawa kwa maisha na ndoa naye. Yote haya yana maana kuwa mwanamke anaweza tu kupata mtoto akiwa na umri wa miaka 30 kuelekea juu.

Wanawake wanaofika umri wa miaka 40 wanakabiliwa na tisho la mimba kutoka, au hata kutoshika hiyo mimba na pia watoto wanaozaliwa katika umri huo huwa na matatizo mengi ya kiafya.