7 wakamatwa kwa dhuluma za ngono Misri

Image caption Wiki jana Misri ilifanya dhuluma za kingono kuwa uhalifu ambao adhabu yake ni miaka 5 jela

Wanaume saba wamekamatwa nchini Misri, baada ya kushukiwa kuwadhulumu kiongono wanawake katika sherehe za Jumamosi za kumkabidhi rasmi mamlaka Rais Abdul Fattah al Sisi.

Hatua ya kuwakamata wanaume hao, inakuja baada ya kanda ya video kusambazwa kwenye internet ikionyesha mwanamke akivuliwa nguo na kuvamiwa na genge la wanaume

Haijulikani ikiwa kanda hiyo ilinaswa, lakini walioshuhudia kitendo hicho waliambia BBC kwambwa unyama huo ulitokea Jumapili usiku.

Wiki jana maafisa wa utawala nchini Misri, waliharamisha dhuluma za kingono na kuufanya uhalifu kwa mara ya kwanza adhabu yake ikiwa miaka mitano jela kwa watakaopatikana na hatia.