Je ngono huathiri wachezaji uwanjani?

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wadadisi wanasema hakuna utafiti unaoonyesha kuwa ngono huathiri uwezo wa mchezaji

Kunakaribia kukucha Brazil wakati dimba la dunia litakapong'oa nanga.

Lakini kwa mara nyingine swala ibuka wakati huu sio jipya. Je ngono inaathiri au kuimarisha uwezo wa mchezaji kuingiza mabao au kusakata kabumbu vyema uwanjani?

Kuna ushahidi finyu kuwa ngono inaathiri kivyovyote uwezo wa mchezaji uwanjani,sasa je kwa nini dhana hii haindoki vinywani mwa wengi ?

Mexico na Brazil zimewaonya wachezaji wao dhidi ya kujihusisha na ngono kabla ya mchi zao. Wachezaji wa Bosnia Herzegovina pia wameonywa kuwa mashangingi na makahaba na wapenzi wengine hawakaribishwi kambini.

Lakini Marekani imekuwa huru kidogo, kwamba wachezaji hawana vikwazo vyovyote. Mwaka 2010, timu ta Argentina ilikuwa huru kujihusisha kingono walivyotaka wachezaji ila matokeo yalikuwa duni kiasi cha kocha Diego Armando Maradona kufurushwa kama kocha wa timu hiyo.

Tabia ya wachezaji kingono wakati wa michuano ya kombe la dunia, imejulikana miaka nenda miaka rudi. Vyombo vya habari vimekuwa vikibugia taarifa za kila aina kuhusiana na ngono na wachezaji wakati wa michuano ya kimataifa kama hii.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kocha Sven aliwaruhusu wachezaji kama Beckham kuandamana na mkewe Brazil

Timu ya England mnamo mwaka 2006 ilitajwa kama sarakasi baada ya meneja wa timu hiyo Sven Goran Eriksson kuruhusu wake wa wachezaji David Beckham na Ashley Cole kuambatana na waume wao.

Miaka minne baadaye Fabio Capello aliwaonya wachezaji dhidi ya kujihusisha na ngono wakati wa mechi nchini Afrika Kusini.

Inafahamika vyema miongoni mwa wataalamu wa maswala ya michezo kuwa ngono haitahiri hali ya mchezo wa mchezaji bora tu mchezaji aweze kupata leope la usingizi.

Lakini dhana hii ya ngono kuathiri wachezaji kabla ya mchezo haipo tu kwenye soka bali pia riadha.

Mwanariadha daima alikuwa akisema, Linford Christie kufanya tendo la ndoa kabla ya mashindano ilifanya miguu yake kulegea.

Image caption Baadji timu zimewaonya wachezaji wao dhidi ya kushiriki ngono wakati wa michuano Brazil

Naye mchezaji tennis wa zamani Ujerumani Boris Becker naye aligonga vichwa vya habari alipokwenda kinyume na agizo la kocha wake kwamba ajizuie na ngono.

Kadhalika mwanamasumbwi Carl Froch alijizuia na ngono kwa miezi mitatu kabla ya kumshinda George Groves katika shindano lao la mimataifa.

Hoja hii bila shaka haitapata jibu leo ikiwa kweli ngono huathiri uwezo wa mchezaji, mwandishi wa habari za michezo Hunter Davies anadhani kuwa mjadala huu huwa ni gumzo tu ambalo watu wanapenda kupiga.