Makahaba Brazil wawalenga wachezaji wa England

Image caption Biashara ya ukahaba imenoga kutokana na kufanyika kwa kombe la dunia nchini humo

Wanawake nchini Brazil wanaanza kujihuisha na biashara ya ukahaba huku wakiwalenga wachezaji wa England.

Wasichana wanaofanya kazi katika danguro la Vila Mimosa iliyoko Rio wanatoa huduma kwa gharama ya chini, 'spesheli' kwa mashabiki wa Uingereza 'kwa sababu wamesafiri kutoka mbali sana'.

Makahaba wanaofanya kazi katika danguro kubwa zaidi nchini Brazil watatoa huduma spesheli kwa mashabiki wa Uingereza, muda mfupi tu kabla ya kung’oa nanga kwa michezo mikubwa zaidi ya soka ulimwenguni.

Wakati michezo hiyo ikianza katika taifa ambalo kandanda inaenziwa mno, takriban wasichana 4,000 wa Vilka Mimosa iliyoko Rio wako tayari kuwapokea wageni wengi kutoka kwenye mataifa 32 yatakayoshiriki Kombe la Dunia.

Wengi wanawaona mashabiki wa Uingereza kama njia ya kupata kipato zaidi, huku wengine wakianza kuifanya biashara hiyo kwa sababu tu ya mashindano hayo.

Wasichana hao watalipisha Euro 16 pekee – ili kufanya mapenzi kwa muda wa nusu saa, huku wengi wakiamini wanaweza kutafuta pasipoti ili kuenda kuishi na waingereza.

Image caption Wengi wa makahaba walijifunza kiingereza kabla ya michuano hiyo ili kuweza kuwasiliana

Huku akiwa amevalia sketi iliyokolea rangi ya bluu, Mel, mama mwenye watoto wawili anasema: “natamani kukutana na mwanamume kutoka taifa la Uingereza, natamani kupanua mtazamo wangu. Nilikuwa kahaba kuanzia majuma matatu yaliyopita. Najua kutakuwa na desturi zingine nyingi wakati wa Kombe la Dunia.

Natumai kupata pesa hizo ili kuisaidia familia yangu, kulipa kodi na bili.

Tunawasubiri waingereza, siwezi kuzungumza lungha yao lakini tutawasiliana kwa njia ninayoijua.”

Vila Mimosa iko karibu na kichinjio na soko la nyama, na nyuma ya barabara hiyo kuu ni maskani yenye mitaa mingi ambapo wasichana hao hufanyia biashara yao. Baa zote 100 katika eneo hilo zina nambari, huku Mel akifanya kazi katika baa nambari 62 kuanzia saa 2 usiku hadi saa 2 asubuhi.

Katika barabara iliyoko nje ya baa hio, wafanya biashara wanapika maharagwe pamoja na supu ya nyama huku wageni pia wakipata fursa ya kunywa 'Mocoto', kinywaji kinachotengenezwa kwa kuchemsha miguu ya Ng’ombe.

Huku mapato ya jumla kwa mananchi wa kawaida yakiwa chini ya Euro 200 kwa mwezi, makahaba hao huweza kupata hadi kufikia mara nne ya mapato hayo. Katikati mwa eneo hilo lenye madanguro, wanawake walio nusu uchi hucheza au kusimama kwa foleni ndefu ili kuonekana na wageni wanaopita.