Msichana mwingine ajinyonga India

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wanawake wa India wapinga ubakaji ambao umekithiri mno India

Msichana mmoja mwenye umri mdogo amepatikana akining'inia mtini Kaskazini mwa India.

Familia ya msichana huyo mwenye umri wa miaka 19, inasema kuwa alibakwa kabla ya kunyongwa na kwamba mwili wake unafanyiwa uchunguzi.

Polisi wanafanya uchunguzi kuhusu tukio hilo ambalo lilijiri katika jimbo la Uttar Pradesh, ambapo wasichana wengine wawili walijinyonga baada ya kubakwa.

Polisi wa mkoa huo pia wanachunguza kifo cha mwanamke mmoja kilichotokea hapo jana Jumatano, ambaye kulingana na familia yake alijinyonga baada ya kubakwa.

Mkuu wa mawaziri wa jimbo hilo anatarajiwa kukutana na waziri mkuu Narendra Modi hii leo huku shutuma zikiendelea dhidi ya mamlaka kushindwa kukabiliana na swala la uhalifu dhidi ya wanawake.

Tukio la wasichana wawili waliobakwa na kisha kuuawa katika hali sawa mwezi jana ilizua gadhabu kuu mwezi jana. Wadadisi wanasema matukio zaidi sasa yanaripotiwa kwa polisi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wasichana wengine walipatikana wakiwa wamejinyonga baada ya kubakwa mwezi jana

Ghadhabu hiyo imesababisha visa vingi zaidi vya ubakaji vinavyotokea kuripotiwa kwa polisi pamoja na vyombo vya habari kuweza kuviangazia.

Uttar Pradesh, ndilo jimbo lenye idadi kubwa zaidi ya watu nchini India, likiwa na watu 200 , pia ni nyumbani kwa idadi kubwa ya watu masikini na wanawake wa tabaka la chini na lenye kudharauliwa. Wao ndio walio katika hatari kubwa ya kushambuliwa.

Mwili wa mwathiriwa wa hivi karibuni ulipatikana katika kijiji kimoja katika jimbo la Moradabad, sio mbali sana kutoka mji mkuu Delhi.

Waandamanaji waliandamana katika jimbo la Uttar Pradesh kwa hasira mwezi jana.

Mnamo Jumatano, mwanamke mwenye umri wa miaka 44 alipatikana akining'inia mtini katika eneo la Bahraich.

Polisi wanasema kuwa alikuwa ametishiwa na wakazi kwa kuuza pombe katika eneo hilo huku familia yake ikidai kuwa alibakwa na genge la watu kabla ya kunyongwa.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii