Nigeria yaomba ujuzi kutoka Sri lanka

Image caption Wanajeshi wa Sri lanka wakiwavizia waasi wa Tamil Tigers

Waziri wa Ulinzi nchini Nigeria amesema kuwa wanasomea ujuzi wa kijeshi uliotumiwa na wanajeshi wa Sri-lanka kuwashinda wapiganaji wa Tamil Tigers katika vita vyake dhidi ya kundi la wapiganaji wa Boko Haram.

Jeshi la Nigeria limekuwa likifanya mazungumzo na ujumbe kutoka Sri-lanka.

Rais wa Nigeria Goodluck Johnathan ameshtumiwa kwa kushindwa kukabiliana na kundi hilo.

Kundi hilo limewauwa maelfu ya raia katika mashambulizi ya miaka mitatu kabla ya kuwateka nyara zaidi ya wasichana wa shule 200 mnamo mwezi Aprili..

Mkuu wa jeshi la angani nchini Nigeria Alex Badeh amesema kuwa wanajaribu kutumia mbinu zilizotumiwa na Sri lanka ikiwemo vifaa vyote vya jeshi la Nigeria.