Leo Uingereza na Italy kumenyana

Image caption Wachezaji wa Uingereza

Siku ya tatu ya michuano ya kombe la dunia inaanza baadaye hii leo huku mechi inayongojewa kwa hamu na mashabiki wengi wa soka ikiwa ile ya Uingereza dhidi ya Italy.

Timu hizo za bara Ulaya zitakutana katika uwanja wa mji wa Manaus katikati ya msitu wa Amazon.

Katika mechi nyengine Colombia itakabiliana na Ugiriki huku Uruguay nayo ikichuana na Costa Rica.

Hapo jana miamba ya soka duniani ambayo ndio bingwa mtetezi wa kombe la dunia Uhispania, ilipata kichapo cha mabao matano dhidi ya Uholanzi katika mechi ya kusisimua iliotawaliwa na Uholanzi.

Vilevile Mexico iliibwaga Cameroon kwa bao moja kwa bila kabla ya Chile kuichapa Australia mabao matatu kwa bila.