Taleban lawakata vidole waliopiga kura

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raia waliopiga kura nchini Afghanistan wakatwa vidole

Maafisa nchini Afghanistan wanasema kuwa watu 11 wamefariki akiwemo mwangalizi mmoja wa uchaguzi baada ya gari lao kazkazini mwa taifa hilo kukanyaga bomu lililotegwa barabarani siku moja tu baada ya kuanza kwa uchaguzi wa urais wa raundi ya pili.

Katika tukio jengine kundi la Taleban liliwakata vidole baadhi ya raia kama adhabu ya kushiriki katika uchaguzi nchini humo.

Zaidi ya watu 60 wameuawa na wanamgambo hao katika misururu ya mashambulizi wakati wa raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.

Raia wa taifa hilo wanachagua kati ya aliyekuwa waziri wa maswala ya kigeni Abdulla Abdulla na Ashraf Ghani ambaye aliwahi kuhudumu kama waziri wa fedha.

Wagombea wote wameahidi kuimarisha uhusiano na mataifa ya magharibi mbali na kukabiliana na ufisadi.