Palestina yalaumiwa kwa utekaji nyara

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwanajeshi wa Israel akipiga doria

Waziri mkuu nchini Israel Benjamin Netanyahu amelishtumu kundi la wapiganaji wa hamas kutoka Palestina kwa kuwateka nyara vijana watatu wa Israel ambao walitoweka katika eneo la West bank siku ya Alhamisi .

Amesema kuwa mtu wa kulaumiwa ni rais wa Palestina Mohamoud Abbas ambaye hivi majuzi aliingia katika mkataba na wapiganaji hao.

Jeshi la Israel linawazuia raia kadhaa wa Palestina katika oparesheni ya kuwasaka wavulana hao ambao walionekana mara ya mwisho katika makaazi ya kiyahudi katika ya mji wa Jerusalem na Hebron.

Kundi la Hamas ambalo linadhibiti ukanda wa Ghaza halijakiri kujihusisha na kitendo hicho.

Mwandishi wa BBC mjini Jerusalem ana hofu kwamba swala hilo huenda likaharibu uhusiano kati ya Israel na Palestina ambao umeathiriwa na kubuniwa kwa serikali ya umoja mapema mwezi huu.