Misri yataka Youtube kuondoa kanda ya dhuluma

Image caption Mwanamke aliyeonyeshwa kwenye kanda akibakwa alitembelewa na Rais Al Sisi

Misri imeomba mtandao wa kijamii wa You Tube kuondoa video ya mwanamke akinyanyaswa kimapenzi katika mkutano wa kisiasa Cairo,kumuunga mkono rais aliyechaguliwa hivi majuzi.

Msemaji wa rais Abdul Fattah al-Sisi alisema ombi hilo lilitolewa na ubalozi wa Misri mjini Washington.

Mwathiriwa alimuomba Bw.Sisi kuondoa video hiyo alipomtembelea hospitalini.

You tube bado haijaitikia ombi hilo la kuondoa kanda hiyo.

Video hiyo ambayo inaonyesha mwanamke akivuliwa nguo hadi kuwa uchi na kushambuliwa eneo la Tahrir square, ilienea mitandaoni mapema wiki hii.

Mfululizo wa mashambulizi wakati wa sherehe hizi za hivi majuzi yamelata vurumai.

Kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali kilionyesha rais akiomba msamaha katika hospitali ya jeshi Cairo, kutoka kwa mwathiriwa ambaye hakutajwa.

Mwanamke huyo alionekana akimuomba Bw. Sisi kuondoa video hiyo ya matukio hayo kutoka kwa mtandao uliokuwa ukiisambaza.

"Mwanangu anazimia kila mara anapoiangalia,"alinukuliwa akisea mwanamke huyo.

Haki miliki ya picha b
Image caption Sherehe za kuapishwa kwa Al Sisi

Hapo jumanne ,msemaji wa serikali alisema Sisi aliwaamuru wakuu wa sheria kutengeneza sheria ya kufanya kitendo cha kumshambulia mtu kimapenzi bila makubaliano hatia.

Sheria hiyo inanukuu kuwa wale watakao patikana na hatia ya kuleta vurumai aidha katika maeneo ya umma au ya kibinafsi watafungwa kifungo cha miaka tano na kutozwa faini ya paundi 50,000 za Misri.

Makundi yanayotetea haki za wanawake yamelaumu wakuu serikalini kwa kushindwa kuangazia swala "la unyanyasaji wa kimapenzi

Katika uchunguzi uliofanywa mwaka jana,takwimu zinaonyesha kati ya wanawake kumi,tisa wamewahi kunyanyaswa kimapenzi, kutoka makosa madogo madogo hadi kunajisiwa.

Wanaotetea haki za kibinadamu wameelezea kiwango cha matukio hayo Egypt kuwa ya kushtusha.

Matukio hayo yamezidi toka kupinduliwa kwa serikali ya Hosni Mubarak mwaka wa 2011.