Ujerumani 4-0 Ureno

Haki miliki ya picha AP
Image caption Thomas Mueller ndiye mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mechi moja Brazil

Thomas Muller alifunga mabao matatu na kuisaidia Ujerumani kuishinda Ureno mabao manne kwa nunge.

Mlinzi wa Ureno, Pepe alionyeshwa kadi nyekundu na kuondolewa katika mchuano huo.

Ujerumani, mabingwa mara tatu wa kombe la dunia, walionyesha mchezo wa kiwango cha juu.

Ujerumani ilichukua uongozi pale ambapo Thomas Muller alipopiga mkwaju wa penalti, baada ya Joao Pereira kuchezea vibaya Mario Goetze.

Mart Hummels alifunga bao la pili kupitia kichwa.

Pepe alionyeshwa kadi nyekundu muda mfupi baadaye kwa kosa la kumgonga Muller kwa kichwa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Pepe alionesha kadi nyekundu baada ya kumgonga kichwa Mueller

Muller alifunga bao la tatu, ambalo lilikua lake la pili katika mchuano huo, kwa mkwaju wa kutoka karibu na lango.

Katika dakika ya 77, Thomas Muller aliongeza bao la nne la Ujerumani na kufanya idadi ya mabao yake katika mchuano huo kuwa matatu.

Muller anakuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mechi moja, kwenye kombe hili la dunia, mwaka 2014.

Kufuatia ushindi huu, Ujerumani inaongoza kundi hili kwa alama tatu.