Nigeria 0-0 Iran

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiungo cha kati cha Nigeria John Obi Mikel

23:50 Hii ndiyo mechi ya kwanza kukamilika ikiwa ni sare tasa katika dimba hili huko Brazil.

23:50 Mechi imekamilika Nigeria 0-0 Iran

23:48 Iran wajipatia Freekick kuelekea lango la Nigeria

23:48 Kona kuelekea lango la Iran

23:46 Obi mikel aangushwa

23:45 Nigeria 0-0 Iran 87''

23:44 Iwapo mechi hii itakamilika ikiwa timu hizi hazijafungana hii ndiyo itakayokuwa mechi ya kwanza ya kombe hili la Dunia kukamilika ikiwa matokeo ni sare tasa.

23:43 Dakika 5 za mechi zimesalia .Nigeria 0-0 Iran

23:42 Nigeria 70%- Iran 30%

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Nahodha wa Nigeria Vincent Enyeama

23:40 Odemwinge akosa nafasi ya wazi ,,,,,lakini refarii anapuliza kipenga

23:38 Dakika kumi tu zimesalia katika mechi hii baina ya Nigeria na Iran.

23:33 Andranik anaonyeshwa kadi ya njano ya kwanza kwenye mechi hii.

23:25 Emenike anaangushwa na kuna ishara zote Kocha Stephen Keshi atamuondoa Azeez nafasi yake ichukuliwe na Odemwingi.

23:25 Obi Mikel anangushwa na inakuwa ni Azeez anayeupiga

23:24 Mashabiki wanawazomea wachezaji wao kwa kukosa makali mbele ya lango.

23:24 Emenike anapeana Freekick kwa Iran

23:22 Kona kwenda kwa lango la Nigeria

23:22 Freekick Reza Ghoochanneijhad (Iran)

23:20 Emmanuel Emenike !

23:15 Nigeria itafunga mechi za mchujo kwa mechi ngumu dhidi ya Argentina .

23:14 Nigeria imeratibiwa kuchauna dhidi ya Bosnia katika mechi ijayo.

23:14 Nigeria haina Budi kufunga bao katika mechi hii iwapo inapania kusonga katika mkondo wa pili.

23:12 Kona inayopigwa na Azeez lakini kipa wa Iran Haghighi anaipokea kama zawadi

23:10 Freekick kuelekea Iran

23:10 Shola Ameobi achukua nafasi yake Victor Moses kunako dakika ya 52'

23:04 Patience Esther Mwikali kutoka kenya anaitakia Nigeria ushindi wa mabao 4-0 Iran

23:03 Kipindi cha pili kinaanza huko Curitiba Nigeria 0- 0 Iran

22:45 Zuhura Iwodiyah kutoka Tanzania anasema Iran atashinda hii mechi

22:45 Rodrick Kakwaya kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam analalamikia safu butu ya mashambulizi ya Nigeria hakuna mashuti makali kwenye lango la Iran

22:45 Siraji Ijaga kutoka Mbale Uganda anaitakia Iran ushindi wa 2- 1 Nigeria.

22:45 Toa maoni yako kwenye mtandao wa Facebook tafuta BBCSwahili hisha ubofye like na tujadiliane.

22:45 Nigeria ilitawala kipindi cha kwanza asilimia 69% Iran 31%

22:45 Hii ndiyo mechi ya pili kutimia muda wa mapumziko timu zote zikwa sare tasa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mashabiki wa Iran

22:45 Mwisho wa kipindi cha kwanza Nigeria 0-0 Iran

22:45 Licha ya kufanya wimbi baada ya wimbi la mashambulizi Nigeria imeshindwa kuvunja safu ya ulinzi ya Iran

22:45 Dakika mbili za ziada katika mechi hii ambayo bado ni sare tasa kati ya Nigeria na Iran

22:39 Victor Moses atekeleza wimbi lingine la mashambulizi kwa msaada wa Obi Mikel

22:32 Iran yapata kona yake ya kwanza na inambidi Vincent Enyeama kufanya kazi ya ziada kunusuru Super Eagles .

22:31 Kipa wa Iran lireza Haghighi anautema na inakuwa Kona.

22:30 Ramon Azeez aangushwa ni Free Kick kuelekea lango la Iran.

22:28 Joseph Yobo kuchukua pahala pake Ogenyi Onazi ambaye anaonekana anamaumivu

22:25 Handball Victor Moses

22:21 Kiungo wa Super Eagles Godfrey Oboabona aondolewa uwanjani kupata matibabu

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Baada ya dakika 20 Nigeria 0-0 Iran.

22:21

22:17 Matokeo bado ni Nigeria 0-0 Iran dakika ya 17 ya mechi zimekamilika hapa katika uwanja wa Baixada ulioko Curitiba

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Timu ya Iran

22:11 Ogenyi Onazi anauguza jeraha

22:07 Ogenyi Onazi ajaribu kufanya mashambulizi katika lango la Iran lakini kipa lireza Haghighi anaupangua.

22:06 Nigeria yapata kona ya kwanza inayochukuliwa na Victor Moses

Haki miliki ya picha
Image caption Mashabiki wa Iran kabla ya mechi

22:02 Victor Moses amjaribu kipa wa Iran Haghighi

21:58 Iran ambao ni mabingwa mara tatu barani Asia wanaorodheshwa katika nafasi ya 43 katika orodha ya FIFA.

Image caption Nigeria ni mabingwa wa Afrika

21:57 Super Eagles inaorodheshwa ya 44 katika orodha timu bora ya Fifa.

21:56 Mabingwa wa Afrika Super Eagle ya Nigeria wanakabiliana na mabingwa wa Asia Iran

21:55 Timu za Iran na Nigeria zinaingia uwanjani tayari kwa mechi yao ya ufunguzi wa kampeni ya kuwania fainali za kombe la dunia huko Brazil.