Ubelgiji 2-1 Algeria

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Algeria iliongoza kwa muda mrefu lakini ikafungwa mabao 2 katika kipindi cha pili.

Wachezaji wa akiba, Marouane Fellaini na Dries Mertens waliisaidia Ubelgiji kupata ushindi muhimu dhidi ya Algeria katika mechi yao ya ufunguzi wa kombe la dunia huko Brazil.

Wawili hao walimarisha sifa za Ubelgiji kuwa moja ya timu bora katika michuano hii ya kombe la dunia, walipofunga mabao mawili na kuifanya timu yao kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu bora kutoka Afrika; Algeria.

Kwa mashabiki wengi, Ubelgiji ilionekana kuwa moja ya timu ambazo zitashamiri huko Brazil hata hivyo iliwalazimu kusubiri hadi dakika ya 70, Ubeljiji kusawazisha bao la mapema la the Desert Foxes ambao walipata bao la penalti katika kipindi cha kwanza kupitia mchezaji Sofiane Feghouli.

Fellaini alifunga bao la kwanza; kwa kichwa katika dakika ya 70.

Mertens naye akafunga la pili dakika kumi baadaye katika dakika ya 80 baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa Eden Hazard.

Kevin De Bruyne alichangia vilivyo katika kupatikana kwa mabao yote ya Ubelgiji na bila shaka mkufunzi wa Ubeljiji, Marc Wilmotsatakuwa na kila sababu ya kufurahia alama hizo tatu kutoka kwa mechi ambayo ilionekana kuwa imemponyoka

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ubeljiji 2-1 Ageria

Ubeljiji ilionekana kuwa goigoi katika kipindi cha kwanza hata ingawa ilikua na sehemu kubwa ya utawala wa mpira katika mechi hiyo.

Hazard na De Bruyne walikuwa na nafasi nyingi, ila safu ya ulinzi wa Algeria uliwazuia kumpitishia mshambulizi Romelu Lukaku mpira.

Madjid Bougherra na Rafik Halliche walilinda eneo la penalti la Algeria na kuyazuia mashambulizi ya wabeljiji .

Kufikia dakika ya 65, Wimots alikua amefanya mabadiliko mengine mawili; Divork Origi aliingia katika nafasi ya Lukaku naye Fellaini kwa upande wa Mousa Dembele.

Origi alipata nafasi nzuri pia, mapema baada ya kuingia kwake lakini kipa, M’Bolhi akausimamisha mkwaju wake wa chini.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mfungaji bao la Ubeljiji Fellaini

Fellaini ndiye alileta tofauti mchezoni alipougonga mkwaju wa De Bruyne kwa kichwa hadi wavuni.

Wachezaji wa akiba walioingizwa na Wilmots walizidi kushambulia naye Mertens akafunga la pili dakika kumi baadaye.

Hili liliwafanya wabeljiji kutegemea mikwaju ya kutoka mbali kutekeleza mashambulizi yao.

Axel Witsel alimjaribu kipa wa Algeria, Rais M’Bolhi na mkwaju mmoja wa kutoka umbali wa yadi 25.

Timu zote zilipoteza nafasi nzuri kupitia mikwaju ya kona.