Polisi walazimishwa kuishi pamoja Kenya

Image caption Polisi walizimishwa kuishi pamoja katika vyumba vyao

Kitengo cha utendakazi cha askari polisi Nchini Kenya kimekumbwa na shida ya ukosefu wa makazi.

Hali imekuwa mbaya sana katika ski za hivu punde kiasi ya kuwa maafisa wa kike na wenzao wa kiume, wamelazimika kutumia kwa pamoja vyumba vyao vichache.

Hili limetokea baada ya zaidi ya maafisa wapya 7,000, kuingizwa katika kitengo hicho miezi miwili iliyopita na kuiongeza idadi ya maafisa wa polisi nchini Kenya kwa asilimia 10.

Hali inaweza zidi kudorora mwaka ujao ikiwa vyumba vipya havitapatikana kwa haraka kwani maafisa wengine 10,000 wataapishwa kujiunga na Idara ya polisi kuhuidumia wananchi na kulinda usalama .

Mpango huo wa kupanua kitengo hicho, ulizinduliwa bungeni na katibu wa fedha Henry Rotich alipoisoma bajeti ya mwaka 2014/2015, juma lililopita.

Kuishi kwenye vibanda

Image caption Polisi nchini Kenya walizimishwa kuishi pamoja katika vyumba vyao

Katika taarifa ya makamanda wa majimbo iliyoonyeshwa wanahabari, maafisa waliamrishwa kuwakaribisha wenzao wapya katika vyumba vyao wanamoishi pamoja na familia zao.

Hii inamaanisha kuwa kurutu anakaribishwa kwa chumba anakoishi Askari na mkewe na familia yake .

“maafisa wengine wanawazuia maafisa hawa wageni kuingia katika nyumba zao na kusababisha hali ngumu kwao.

Maafisa wa polisi watakaokiuka amri hiyo watachukuliwa hatua za kinidhamu . Taarifa hiyo ilisema.

Maafisa waliozungumza na wanahabari, kwa masharti ya kutotajwa walisema kuwa amri hiyo itawanyima faragha na wake zao mbali na kuibua uhasama na ugomvi katika familia zao.

Mgogoro huo uliwalazimisha maafisa hao wapya kutafuta makao katika vibanda viliyo katika vituo vya polisi kwa hofu ya kuvunja nyumba za wenzao .

Maafisa hawa wapya walitawazwa kuwa makonstebo mwezi Aprili na kuchukuliwa katika vitengo vya Polisi ,Kitengo cha Jinai na kikosi cha kupambana na ghasia.