Mwalimu Mkenya katika kombe la dunia Brazil

Imebadilishwa: 20 Juni, 2014 - Saa 15:09 GMT

Kocha Marwa

  • Aden Marwa mwenye umri wa miaka 37 ni mmoja wa marefa wanaochezesha michuano ya kombe la dunia nchini Brazil. Ni refa wa kwanza mkenya kuwahi kuchezesha katika dimba la dunia
  • Marwa alianza kucheza mpira baada ya kumaliza shule ya upili, kabla ya hapo alienzi sana kucheza mipira ya mikono.
  • Kuanza kushiriki soka kwa Marwa kulikuja na baraka zake kama anavyosema mwenyewe, mataji haya ameyapokea baada ya kuchezesha mechi kadhaa barani Afrika. Licha ya kusifika katika kanda nzima, Marwa pia huchezesha mechi za nyumbani
  • Marwa anajivunia kuwa refa wa kwanza mkenya kuwahi kuchezesha mechi za kombe la dunia. Hii ndio jezi ayakalovaa akiwa uwanjani. ''Nikufahamishe tu kuwa mimi sina timu ninayopendelea, nitachezesha mechi zote kwa uwazi,'' asema Marwa ambaye anasema kwamba anapenda sana rangi hii ya jezi lake.
  • Mbali na kazi yake ya urefa, Marwa ni mwalimu wa shule ya upili ya Komotobo Magharibi mwa Kenya. Anafunza Kemia na hesabu na yeye ndiye kiongozi wa michezo katika shule
  • Marwa anatumai kuwa nafasi hii aliyoipata katika kombe la dunia itawapa motisha vijana kuweza kutumia vipaji kujiimarisha au kujiendeleza.

Washiriki katika kombe la dunia huwa na fahari kubwa kujihusisha katika michuanbo hiyo katika namna yoyote ile.

Na ndivyo ilivyo kwa Mkenya Bwana Aden Marwa ambaye ni mmoja ambaye ameteuliwa kuwa miongoni mwa marefa watakaocheza michuano ya kombe hilo huko Brazil kuanzia wiki hii.

Paul Nabiswa alimtembelea refa huyo msaidizi ambaye vile vile ni mwalimu wa Kemia na Hesabu katika kijiji anachotoka huko Kuria karibu na mpaka wa Kenya na Tanzania.

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.