MSF;Ugonjwa wa Ebola haudhibitiki tena

Image caption Raia anayeugua ugonjwa w Ebola

Afisa mwandamizi wa shirika la madaktari wasio na Mipaka Medicine San Frontiers ameelezea kuwa mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola katika mataifa matatu ya magharibi hauwezi kudhibitika.

Mkurugenzi wa Oparesheni katika shirika hilo Bart Janssens ameliambia shirika la habari la A.P kwamba ugonjwa huo utasambaa hadi katika mataifa mengine iwapo hakutakuwa na mwitikio wa kimataifa.

Ugonjwa wa Ebola tayari umesababisha vifo vya takriban watu 330 nchini Guinea,Sierra leone na Liberia.

Bwana Janssens amesema kuwa shirika la MSF limefikia kikomo cha uwezo wake wa kukabiliana na ugonjwa huo.