Kijiji karibu na Chibok chashambuliwa

Chibok, Nigeria Haki miliki ya picha AFP

Ripoti zinasema kuwa shambulio jengine limetokea katika kijiji kimoja cha kaskazini-mashariki mwa Nigeria, karibu na pahala ambapo wasichana wa shule zaidi ya mia-mbili walitekwa nyara.

Kiongozi mmoja wa kijiji aliiambia BBC kwamba watu waliokuwa na silaha walivamia kijiji cha Koronginim, kama kilomita 14 kutoka Chibok ambako wasichana walitekwa na wapiganaji Waislamu wa kundi la Boko Haram mwezi Aprili.

Alieleza kuwa watu kama watatu waliuwawa na kwamba kijiji hicho kimeteketezwa na moto.

Aliongeza kusema anafikiri washambuliaji walikuwa wapiganaji wa Boko Haram.