Iran:Saudia na Qatar ndio wachochezi

Image caption Wakimbizi nchini Iraq

Rais wa Iran Hassan Rouhani ameyashtumu mataifa yenye utajiri mkubwa wa mafuta katika eneo la mashariki ya kati kwa kutumia fedha zao ili kulifadhili kundi la wapiganaji wa kisunii nchini Iraq.

Huku akielekeza kidole chake cha lawama kwa Saudia Arabia na Qatar ,rais Rouhani ameonya kwamba siku moja sera zao zitawaathiri wenyewe kwa kuwa wanamgmbo hao watazigeukia nchi hizo.

Akizungumza katika kongamano moja la kidini mjini Tehran ,bwana Rouhani amelalamika kuhusu tofauti inayoendelea kuibuka kati ya raia wa kishia na wenzao wa kisuni akisema kuwa hiyo ni kazi ya Israel.

Iran ndio inayoongoza kwa watu wa dhehebu la wa shia, na bwana Rouhani hapo awali amenukuliwa akisema kuwa Tehran haitasita kutetea maeneo ya makumbusho ya wa shia nchini Iraq.

Iran imekuwa ikimuunga mkono waziri mkuu wa Iraq Nouri Al Malik ambaye ni wa dhehebu la kishia.