Wengi waliuwawa Nigeria Jumamosi

Waumini kanisani wakiomba wasichana wa Chibok waachiliwe huru Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Wakazi wa Nigeria wamekuwa wakihangaishwa na Boko Haram kwa muda mrefu sana

Inafikiriwa kuwa watu kadha waliuwawa katika mashambulio yaliyofanywa na wale wanaoshukiwa kuwa wapiganaji Waislamu kaskazini mwa Nigeria hapo jana.

Wakaazi wa huko wanasema wapiganaji wa Boko Haram walikuwapo kwa saa sita, wakiuwa watu na kuchoma moto vijiji.

Inasemekana kati ya waliouwawa ni askari wa usalama.

Baadae wanajeshi na ndege zilipelekwa katika eneo hilo na mtu mmoja aliyeshuhudia tukio hilo, anasema maiti za wapiganaji kadha zimepatikana nje ya vijiji.

Mashambulio hayo yalifanywa karibu na Chibok ambako wapiganaji waliwateka wasichana wa shule zaidi ya 200 mwezi Aprili.