Watu 20 wauwawa Wajir, Kenya

Wajir shambani

Watu kama 20 wameuwawa katika shambulio kwenye kijiji kaskazini-mashariki mwa Kenya.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema watu waliojihami vema, walivamia kijiji cha Gunana katika wilaya ya Wajir Jumapili alfajiri.

Anasema chanzo cha ugomvi ni mzozo baina ya koo mbili, Degodia na Gare.

Ni mzozo wa mpaka baina ya koo hizo ambao wakuu wanautambua, lakini bado hawakuweza kuupatia ufumbuzi.

Ingawa kumewahi kutokea mapambano kati ya koo hizo lakini idadi ya waliouwawa katika shambulio hili ni kubwa.