Korti yawakataza wakristo kutumia neno Allah

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waimini wa kiisilamu wanaamndamana kupinga wakristo kutumia neno Allah

Mahakama kuu nchini Malaysia imetupilia mbali ombi la kanisa Katholiki nchini humo kumuita Mungu "Allah" katika gazeti lao la lugha ya ki Malay.

Kesi hiyo ilianza mwaka 2007 pale ambapo serikali ilitishia kusimamisha huduma za gazeti hilo la kila wiki la kanisa katoliki, The Herald, ikiwa litaendelea kumuita Mungu, Allah.

Walidai kuwa wakristo wanawakanganya waislamu walio wengi na hilo laweza kuhatarisha usalama wa taifa.

Uamuzi huo, ni mojawapo ya mikondo ya mwisho ya kesi za kisheria za kanisa katoliki zilizochukua muda wa miaka saba na ambao umesababisha mashambulizi katika makanisa, majumba ya maombi ya waislamu na pia hekalu la wasikh katika mwaka wa 2010.

Wakristo na wasikh wanadai kuwa wamekuwa wakimwita Mungu, Allah katika lugha za kiMalay na Sansrit kwa muda mrefu sana.

Mahakama nayo imeshikilia uamuzi wao wa awali kuwa jina hilo halifai kuingizwa katika ukristo.

Viongozi wa kanisa wanaogopa kuwa uamuzi huo utasababisha kizingiti kwa washiriki wake milioni mbili.

Mgongano huo kuhusu neno hilo moja umedhihirisha jinsi nchi hiyo yenye dini na kabila tofauti tofauti lilivyogawanyika.

Wanaharakati wa kiislamu wamekua wakishabikia uamuzi huo nje ya majumba ya koti,wengi wao wanaamini kuwa wakristo wanamwita Mungu, Allah, kama njia ya kuwavuta waislamu wajiunge na ukristo, shutma ambazo wakristo wamekana.

Mwanasheria mmoja anayewakilisha kanisa katholiki anashauri kuwa bado wanaweza kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa mahakama.

Pia kuna wakristo wengine wanaoleta chochezi za kisheria kama hizo, dhidi ya uamuzi huo wa serikali.