Sisi hataingilia uamuzi wa mahakama

Haki miliki ya picha
Image caption Wandishi watatu wa Al Jazeera walihukumiwa kiufungo cha kati ya miaka saba na kumi jela

Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi amesema kuwa hataingilia kati uamuzi wa mahakama hata baada ya wito wa kimataifa kufuatia kufungwa kwa wandishi watatu wa kituo cha Al-Jazeera.

Bwana Sisi amesema kuwa utawala nchini Misri ni lazima uheshimu uamuzi wa mahakama na kukomesha shutuma.

Sisi aliyazungumza hayo muda mfupi baada ya serikali ya Australia kumtaka atafute suluhu ya kesi ya mmoja ya waandishi hao Peter Greste.

Waziri mkuu nchini Australia amesema kuwa amesononeshwa na hukumu iliyotolewa mjini Cairo siku ya Jumatatu

Waandishi wa BBC na wale kutoka Al-Jazeera kote duniani wamekimya kwa dakika moja kuonyesha uzalendo kwa waandishi hao.

Greste na wenzake watatu walihukumiwa jela kwa tuhuma za kuunga mkono kundi la Muslim Brotherhood na kutangaza taarifa za kupotosha.