Heroin yanaswa Afrika kusini

Image caption Uraibu wa madawa ya kulevya unaongezeka Afrika kusini

Polisi nchini Afrika kusini wamenasa madawa ya kulevya aina ya heroin yenye thamani ya zaidi ya dola milioni 190.

Raia wawili wa China wametiwa mbaroni kwa kuwa washukiwa katika sakata hiyo kubwa inayohusu kunaswa kwa madawa ya kulevya, kuwahi kushuhudiwa katika historia ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la Reuters, maafisa wa polisi pia wamemtia mbaroni raia mmoja wa Afrika kusini katika uvamizi uliofanyika kwenye nyumba moja katika eneo la Kloof lililo kilomita ishirini na tano kutoka mji wenye bandari kubwa Afrika Durban.

"Tulidokezwa na wakaazi wa eneo hilo na maafisa waliivamia nyumba hiyo na kupata kiwango hiki kikubwa cha heroin," alisema msemaji wa polisi Thulani Zwane said.

Afrika kusini ni nchi yenye soko kubwa kwa madawa ya kulevya na kwa mujibu wa baraza la kitaifa kuhusu ulevi na uraibu wa madawa ya kulevya, matumizi yake yanaongezeka.