EU:Junker kutawazwa kama rais mpya

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kiongozi wa chama cha EPP Jean Claude Junker

Viongozi wa muungano wa ulaya wanaokutana katika jiji la Brussels nchini Ubelgiji wanatarajiwa kumtawaza aliyekuwa waziri mkuu wa Luxembourg, Jean-Claude Junker kuwa rais mpya wa tume ya bara Uropa.

Hili latanyika licha ya upinzani mkubwa kutoka Uingereza.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron amesema kuwa haoni uwezekano wake kushinda katika tukio hili, dhidi ya Junker,lakini amesisitiza kuwa atafuata kanuni zake yeye mwenyewe.

Anaamini kuwa Junker anapendelea umoja wa kisiasa na hili laweza kudhuru mabadiliko katika umoja huo wa Uropa.

Pia anapinga jinsi Junker, mwenye umri wa miaka 59 na ambaye ni mkongwe katika alivyochaguliwa.

Amekua mgombea aliyeongoza katika chama cha European Peoples Party (EPP) kilichoshinda uchaguzi wa mwezi uliopita.

Wanacham wa Uingereza wamejiondoa katika chama cha EPP, kwa kuwa tume hiyo inaingizwa na Bunge la bara Uropa, katika siasa za kung'ang'nia mamlaka.

Hata hivyo, wafuasi wa Junker wanaisifu rekodi yake ya kuunda mikakati ya makubaliano na dhamira yake ya kuunganisha bara Uropa.

Chini ya sheria ya makubaliano haya mapya, viongozi wanapaswa kujua matokeo ya kura ya bara Uropa wanapomchagua kiongozi wa tume hiyo.

Bunge litafanya uchaguzi kumchagua kiongozi huyo mwezi ujao.

Cameron anatafuta kuungwa mkono katika uteuzi huo, ambao haswa hufanywa kwa makubaliano.

Hata hivyo, jaribio lake la kumzuia lilipata pigo kubwa juma hili pale ambapo wanaoshirikiana naye walipomgeuka.

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel alikua amempa Cameron matumaini baada ya kukubali kupigia kura swala hilo iwapo hakutakuwa na makubaliano.

Uholanzi na Uswizi, ambao haswa hukubaliana na Uingereza katika maswala mengi, walisema kuwa wanamuunga mkono Junker.