kesi ya Pistorius yaendelea leo

Image caption Oscar Pistorius akilia wakati wa kesi

Kesi ya mauji ya mwanariadha wa Afrika kusini , Oscar Pistorius, inaendelea kusikilizwa leo hii baada ya kipindi cha mapumziko ya wiki sita.

Upande wa utetezi unadai mteja wao alikuwa anaugua mkanganyiko wa akili wakati alipomuua mpenzi wake , Reeva Steenkamp, huko nyumbani kwake hapo mwaka jana.

Wataalamu wa kisaikologia wanatakiwa kumchunguza kubaini iwapo Pistorius alikuwa na akili timamu na hivyo anaweza kuwajibishwa kikamilifu au la kwa kitendo hicho cha kumfatulia risasi msichana huyo mara kadhaa alipokuwa amekimbilia usalama wake kwa kujifungia katika chumba cha kuoga.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Oscar Pistorius na Reeva Steenkamp wakati wa uhai wake.

Pistorius anadai alishuku kimakosa ni mvamizi wala si Reeva.

Ripoti hiyo ya madaktari na wataalam inatarajiwa kumsaidia na kumwelekeza jaji kufanya maamuzi ya busara katika kesi hiyo iliyogonga vichwa vya habari Afrika kusini na kwingi duniani.

Hata hivyo mwandishi wa BBC aliyeko Johannesburg anasema kwa upande mwengine ripoti hiyo ya madaktari huenda isibadili pakubwa maamuzi ambayo yatafanywa kwani hata upande wautetezi wenyewe washakiri kuwa kiwango cha kuchanganyikiwa kiakili cha Pistorious hakikuwa kibaya kiasi cha kutongamua baya na zuri.

Mawakili wa utetezi watakamilisha kutoa ushahidi wao katika siku chache zijazo.

Steenkamp, mwanasheria na mwanamitindo mwenye umri wa miaka 29, aliuawa kwenye tukio hilo mwaka jana siku ya wapendanao ijulikanayo vyema kama Valentine's Day.