Pistorius hana matatizo ya kiakili

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Pistorius amekana madai ya kuua mpenzi wake kwa maksudi

Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius hakuwa na tatizo lolote la kiakili wakati alipomuua mpenzi wake mwaka jana.

Haya ni matokeo ya uchunguzi wa kiakili aliofanyiwa Oscar Pistorius huku kesi yae ikianza kusikilizwa tena nchini Afrika Kusini.

Ripoti hiyo iliwasilishwa baada ya uchunguzi kufanywa kuhusu hali yake ya kiakili wakati alipofanya mauaji hayo mwaka jana.

Mawakili wake walikuwa wamedai kuwa Pistorius aliukuwa anakumbwa na hali ya wasiwasi na kuzongwa na mawazo wakati wa mauaji ya Reeva Steenkamp.

Mwanariadha huyo amekana kumuua kwa maksudi mpenzi wake Reeva Steenkamp akisema kuwa alimpiga risasi kwa bahati mbaya baada ya kupatwa na wasiwasi akidhani jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.

Upande wa mashitaka pamoja na utetezi wamekubali matokeo ya uchunguzi huo.

Upande wa utetezi sasa unasikia ushahidi wake daktari aliyemkata miguu Pistorius, Gerry Versfeld, anayetoa ushahidi kuhusu athari za Pistorius kukatwa miguu.

Upande wa utetezi nao unatarajiwa kumaliza ushahidi wake katika siku chache zijazo.

Bi Steenkamp, alikuwa na umri wa miaka 29, wakati wa mauaji yake Februari mwaka jana.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii