Israel yasema Hamas iliwauwa vijana wake

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Vijana wa Israel waliopatika awakiwa wameuawa

Msemaji wa jeshi la Israel amesema kuwa miili hiyo ilikuwa chini ya miamba iliopo kwenye mji wa west Bank wa Hebron.

Israel imepeleka vikosi vyake katika kijiji cha Palestina cha Hal-hul.

Katika kikao cha dharura cha mawaziri ,waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema vijana hao walitekwa na kuuawa katika mauji aliyosema yamefanywa na wanyama.

Netanyahu amelilaumu kundi la Wapalestina la Hamas, na akaahidi kulipiza kisasi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu

Hamas imekana kuhusika na mauaji hayo kupitia mshauri rasmi wa rais wa Palestina Mahmoud Abbas -Abdallah Abdallah

Mwandishi wa BBC aliyeko mashariki ya kati anasema milio ya mashambulizi ya ndege za Israeli imesikika kote katika ukanda wa Gaza .

Kulikuwa na tetesi kuwa Israeli ingeileng maeneo ya Hamas baada ya kikao chake cha mawaziri cha usalama .

Mji wa Gaza umesalia kuwa ngome kuu ya Hamas na ofisi zake katika eneo hilo zimekuwa zikivamiwa katika kipindi cha zaidi ya wiki mbili na nusu.

vifo vya karibu wapalestina watano vimeripotiwa na mamia ya wapalestina wamekamatwa.