Aokoa dereva kwa kukunja mlango wa gari

Mwanamume mmoja nchini Marekani alimuokoa dereva wa gari ,lililokuwa linateketea kwa kuukunja mlango wa gari hilo kwa mikono yake.

Polisi wamemtaja Bob Renning, mwenye umri wa miaka 52,kama mtu mwenye nguvu za ajabu.

Alianza kwa kuegesha gari lake kando ya barabara kuu mjini Minnesotaili kumsaidia dereva huyo ambaye alikuwa ndani ya gari lililokuwa linateketea.

Bwana Rob aliwaambioa wandishi kuwa haelewi alivyoukunja mlango wa gari hilo kiasi cha kuvunja dirisha la gari.

Polisi walimsifu Rob kwa juhudi zake za uokozi.

"alifanya kitendo cha ajabu , kuukunja mlango wa gari hilo lililokuwa linateketea ili kumuokoa dereva, '' alisema polisi.

Dereva wa gari hilo alisema hakuwa na habari ikiwa kuna mtu alikuwa anamuokoa.

Alipatwa na tatizo la kupumua kutokana na moshi mkubwa uliokuwa unafuka ndani ya gari lake , ingawa aliokolewa kupitia kwa dirisha la mlango huo uliokuwa umevunjwa.