Nicolas Sarkozy afanyiwa uchunguzi

Haki miliki ya picha s
Image caption Sarkozy adaiwa kupoke fedha za kampeni kinyume cha sheria kutoka kwa marehemu Ghadafi

Rais wa zamani wa Ufaransa , Nicolas Sarkozy, amefikishwa mahakamani mjini Paris, kwa tuhuma za kutumia nafasi yake vibaya miongoni mwa tuhuma nyenginezo kuhusiana na makosa makubwa ya uchaguzi.

Sarkozy anajipata tena matatani tangu kupoteza kinga ya kushtakiwa mda mfupi baada ya kupoteza kiti cha urais kwa muhula wa pili , kilichonyakuliwa na rais wa sasa Francois Hollande hapo 2012.

Sarkozy anakana kuwa alipata ufadhili kinyume cha sheria katika uchaguzi huo.

Awali alihojiwa kutokana na tuhuma za kufanya ushawishi kuhusu kesi inayochunguzwa kupata ufadhili wa fedha za kampeni kinyume cha sheria , ikiwemo kupokea fedha kutoka kiongozi wa zamani marehemu Muamar Ghadafi.

Mwanasheria wa Bwana Sarkozy, alihojiwa Jumatatu kuhusu tuhuma za kutafuta taarifa za ndani kuhusu kesi inayomkabili kiongozi huyo wa zamani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sarkozy na mkewe mwimbaji Carla Bruni

Hali ya sasa hivi inaonekana pigo kuu kwa Bwana Sarkozy.

Wachunguzi wanajaribu kutafuta iwapo Bwana Sarkozy, mwenye umri wa miaka 59, ambaye alikuwa rais wa Ufaransa kutoka mwaka 2007 hadi 2012, aliahidi kumpa wadhifa mkubwa jaji wa Monaco, Gilbert Azibert, ikiwa ni shukrani ya kupatiwa taarifa kuhusu uchunguzi unaofanyika dhidi kuhusu fedha aliyoitumia katika kampeni ya uchaguzi.

Wanachunguza madai kwamba Bwana Sarkozy alionywa simu yake ilikuwa inadukuliwa ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa fedha zilizotumika katika kampeni.

Bwana Azibert, mmoja wa majaji waandamizi katika mahakama ya rufaa, aliitwa kuhojiwa Jumatatu. Jaji mwingine Patrick Sassoust, naye pia alihojiwa, kama ilivyokuwa kwa mwanasheria wa Bwana Sarkozy, Thierry Herzog.