Mwindaji akemewa Facebook

Image caption Kendal akiwa na mmoja wa wanyama aliowawinda Afrika kihalali

Kendall Jones ana umri wa miaka 19, kutoka Texas Marekani.

Yuko katika chuo kikuu na zamani alikuwa mpigia debe timu ya michezo, lakini sasa hivi, hafanyi kazi hiyo tena.

Maisha yake yamebadilika kama zilivyo post zake za Facebook.

Kendal siku hizi hujipiga picha na wanyama wakubwa kama vile Simba ambao amewawinda kihalali barani Afrika.

Ukurasa wake wa Facebook umezua hisia kali na amekosolewa sana katika siku chache zilizopita, huku maelfu wakimtaka akome kuwinda barani Afrika.

Lakini Kendal amejitetea na hata kujifananisha na rais wa zamani wa Marekani Theodore Roosevelt, ambaye alianzisha mbuga za wanyama nchini humo.

Nini maoni yako kuhusu kazi ya Kendal?