Bei ya mafuta na umeme yapanda Misri

Haki miliki ya picha AP
Image caption Uhaba wa mafuta nchini Misri

Bei ya mafuta na umeme iliyoongezeka imeanza kutumika nchini Misri huku serikali ikianza kukata ruzuku yake.

Hii ni mbali na kupunguza matumizi ya bajeti yake ili kufufua uchumi ulioathiriwa na mgogoro wa kisiasa wa miaka kadhaa.

Baadhi ya bei za mafuta zinadaiwa kupanda kwa asilimia 78 huku bei ya umeme ikipanda maradufu katika kipindi cha miaka mitano.

Kwa sasa serikali inauza umeme kwa nusu ya gharama ya uzalishaji wake.

Kukatika kwa umeme nchini Misri limekuwa jambo la kawaida na maafisa wanasema kuwa gharama ya juu ya ruzuku imelemaza ukarabati na upanuzi wa mitambo ya kuzalisha umeme.

Waandishi wanasema kuwa kupanda kwa bei ya umeme nchini humo ni hatua mojawapo ya serikali katika kile kinachotarajiwa kuwa marekebisho ya kisiasa kwa ruzuku zinazosimamia Mafuta,Uchukuzi,chakula na kilimo.