Kiongozi wa Brotherhood afungwa maisha

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kiongozi wa Muslim Brotherhood Mohammed Badie [katikati[

Mahakama moja nchini Misri imempatia kifungo cha maisha jela kiongozi wa kundi la Muslim Brotherhood Mohammed Badie na wanachama wengine 36.

Watu hao walipewa hukumu hiyo kwa kuchochea ghasia na kufunga barabara wakati wa maandamano baada ya jeshi kumpindua aliyekuwa rais wa taifa hilo Mohammed Morsi mwaka uliopita.

Bwana Badie tayari anakabiliwa na hukumu nyengine ya kifo kutoka kesi nyengine.

Mahakama hiyo ya mjini Cairo pia iliwahukumu vifo wanachama wengine kumi wa kundi la Muslim brotherhood.

Makundi ya haki za kibinaadamu yamekosoa misururu ya hukumu za kifo nchini Misri yakisema zilishinikizwa kisiasa.