'Hatujatoroka', wasema waasi wa Ukraine

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiganaji wanaounga mkono Urusi

Wapiganaji wanaounga mkono Urusi Mashariki mwa Ukraine wamepinga ripoti kwamba wameitoroka ngome yao kuu ya mji wa Slovianski.

Waziri wa mswala ya ndani wa Ukraine amesema kuwa idadi kuu ya waasi hao imeondoka lakini akakiri kwamba wapiganaji wengine bado wamesalia mjini humo.

Vikosi vya Ukraine vilianzisha mashambulizi dhidi ya wanamgambo hao baada ya siku kumi za kusitishwa kwa vita.

Rais wa Ukraine Petro Poroshenko amesema kuwa yuko tayari kusitishwa kwa vita lakini hakuna thibitisho lolote la mazungumzo mapya.

Image caption Rais wa Ukraine Petro Poroshenko

Waziri wa maswala ya ndani Arsen Avakov alisema katika mtandao wa facebook kwamba idadi kubwa ya wapiganaji hao waliondoka slovianski lakini kwamba wengine wako mjini humo ambao haujatekwa na vikosi vya serikali.

Amesema kuwa ripoti za ki-intelijensia zinasema kuwa kamanda wa vikosi vya Jamhuri ya watu wa Donetsk Igor Strelkov ni miongoni mwawale wanaoondoka ,lakini hilo halijathibitishwa.

Awali kulikuwa na ripoti kwamba wapiganaji wanaounga mkono Urusi waliondoka katika mji wa Sloviansk, ambayo ni miongoni mwa ngome zao kuu .

Imedai kuwa msafara wa wapiganaji hao na silaha zao ulionekana ukielekea katika mji jirani wa Kramatorsk.