Washambuliaji wauwawa magharibi Uganda

Image caption Awali kulikuwa na tahadhari ya kutokea mashambulizi Uganda

Askari wa usalama wa Uganda wanasema kuwa watu kadha wameuwawa katika shambulio lililofanywa na watu waliokuwa wamejihami, Magharibi mwa nchi.

Askari polisi kama watatu piya walikufa wakati vituo vya polisi na jeshi viliposhambuliwa.

Inasemekana kuwa askari wa Uganda wamewauwa washambuliaji zaidi ya 40 huku raia na polisi 18 wakiuawa pia.

Haijulikani nani anahusika na ghasia huko Bundibugyo katika wilaya ya Kasese, ambayo inapakana na Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Baadhi ya ripoti zinasema ghasia hizo ni za kikabila na nyengine zinasema zinafanya na makundi ya waisilamu.