Serikali yadhibiti miji miwili Ukraine

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Waasi mashariki mwa Ukraine wamejipanga upya katika maeneo mengine

Maafisa katika mji mkuu wa Ukraine, Kiev wanasema vikosi vya serikali vimeyadhibiti miji miwili zaidi kutoka kwa waasi wanaoiunga Urusi mkono mashariki mwa nchi hiyo.Hii inafuata hatua ya kudhibitiwa kwa ngome mbili kuu za waasi hao siku ya Jumamosi.

Wakati huo huo mamia ya watu wamekusanyika kwa mkutano katika mji uliopo mashariki Donetsk katika kuwaunga mkono waasi.

Kwa mujibu wa mtandao wa rais mpya wa Ukraine, Petro Poroshenko, bendera imepandishwa katika miji ya Artyomivsk na Druzhkivka.

Miji hiyo haina uzito kama vile Sloviansk, uliodhibitiwa siku ya Jumamosi.

Lakini hatua ya kuyadhibiti upya miji hiyo inaashiria kuwa kasi inaongezeka kwa upande wa vikosi vya serikali.

Wapiganji waasi wamejipanga upya katika maeneo mengine, ikiwemo katika mji mkuu wa eneo hilo, Donetsk.

Mami kadhaa ya watu waliandamana katika bustani kuu ya mji huo katika kuuga mkono uasi huo.

Maafisa mjini Kiev wanasema wataendelea na mashambulio yao na wamekataa kuidhinisha makubaliano mapya ya kusitisha mapigano ya upande mmoja.