Israel yafanya mashambulizi zaidi Gaza

Haki miliki ya picha Reuters

Israel imefanya mashambulizi zaidi katika ukanda wa Gaza kufuatia shambulizi la makombora lililofanywa na kundi la Hamas Jumatatu.

Mashambulizi hayo yalisababisha vifo vya wa-Palestina kumi na watano huku wanawake wawili na mtoto wakiripotiwa kujeruhiwa.

Kundi la Hamas lilifanya mashambulizi likidai Waisraili walifanya ukatili kwa kuwaua wapiganaji watano wa Hamas.

Israil ilikana madai hayo na kusema imezindua operesheni hiyo ya anga ili kukabiliana na urushaji makombora kutoka Gaza. Aidha, Israeli ilisema itatumia majeshi elfu moja na mia tano maalum kuendeleza na kueneza operesheni hiyo siku za usoni.

Hofu imetanda kufuatia mauaji ya vijana watatu wa kiyahudi na mpalestina.

'Gharama kubwa'

Haki miliki ya picha Reuters

Jeshi la Ulinzi la Israeli, IDF imezindua operesheni hiyo maarufu kama Operation Protective Edge huko Gaza dhidi ya Hamas.

Imetuma vikosi zaidi mpakani mwa Gaza katika harakati za kulinda raia wa Israeli, ikidai mashambulizi hamsini yalitekelezwa usiku.

Hata hivyo baraza la mawaziri nchini Israeli limesitisha operesheni ya nchi kavu kwa sasa.

Viongozi wameshauri miji iliyoko kilomita arobaini karibu na eneo hilo lililoshambuliwa kufunga shule pamoja na maeneo ya kujitumbiza.

Jeshi linadai makombora zaidi yalirushwa kutoka Israeli kwenda Gaza, huku Hamas ikidai Israeli ililenga nyumba mbili na shule mbili zinazotumika na wanamgambo kote Gaza