20 wauawa katika shambulio la anga, Gaza

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption watu 20 wauawa katika shambulio la Israel

Mashambulio ya anga yaliyofanywa na Israel yamewaua zaidi ya watu 20 katika eneo la Gaza, wakiwemo raia. mashambulio hayo yanatazamiwa kuwa mwanzo tu wa oparesheni kubwa inayopangwa kufanywa na Israel.

Maafisa wa Palestina wanasema kuwa kiongozi mmoja wa kundi la wapiganaji wa kiisamu la 'Islamic Jihad' ameuawa baada ya makaazi yake mjini Beit Hanoun kaskazini mwa Gaza kulipuliwa kwa bomu.

Kiongozi huyo, Hafez Hamad aliuliwa pamoja na watu wengine watano wakiwemo wazazi wake na ndugu zake wawili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption wapalestina nao warusha makombora Israel

Awali wapiganaji wa kipalestina walirusha makombora ndani ya Israel wakilenga miji ya Haifa, Tel Aviv na Jerusalem.

Jeshi la Israel linasema kuwa limedingua kombora moja kutoka anga ya mji wa Tel Aviv huku maafisa mjini Jerusalem wakidai kuwa kombora limelipuka katika uwanja mdogo nje ya Jerusalem.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Benjamin Netanyahu wa Israel

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kuwa wapiganaji wa Hamas wanatumia raia wa kipalestina kama ngao kwa hivyo wao ndio wa kulaumiwa kwa vifo vya raia hao.

Hai a taharuki imetanda nchini Israel baada ya vijana 3 wa nchi hiyo kuuwa katika ukingo wa Magharibi mwezi uliopita.

Tukio hilo lilijibiwa na Israel kwa kumuua kijana mmoja wa kipalestina