Mapenzi yanoga licha ya kipigo Brazil

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Beatriz Groxco na Federico Astorga

Wengi wamekiita kipigo cha karne baadhi wakasema kilikuwa kimbunga cha magoli, yote tisa, kumi ni kwamba majonzi yalijaa Brazil baada ya timu yao kupokea kipigo kutoka kwa Ujerumani katika nusu faiunali ya kwanza ya kombe la dunia.

Lakini licha ya huzuni wote huo, kunao mashabiki ambao wameitumia fursa ya kuwepo kombe la dunia Brazil kujinawirisha kimapenzi.

Itakushangaza kuwa mapenzi yamenoga kati ya mashabiki wa timu hasimu ambao wamepata penzi tamu licha ya uhasimu wa timu na nchi.

Kwa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 25 raia wa Brazil, Beatriz Groxco, ametupilia mbali uhasimu wake wa kihistoria na Argentina kwa kukutana na mtu ambaye sasa amekuwa mpenzi wake Federico Astorga, shabiki wa Argentina.

Federico alikuwa njiani kuelekea Sao Paulo kwa mechi alipokatizia safari yake mjini Curitiba nyumbani kwa Beatriz. Tangu hapo mapenzi yamewanogea.

Walikutana wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo tarehe 12 Juni, siku hiyo ilikuwa siku ya wapendano Brazil, hawajaachana tangu hapo.

"nilikuwa naelekea mjini ambako kuna baa nyingi wakati aliponiomba kumuelekeza, '' asema Beatriz.

''Mashabiki wa Brazil, huwakejeli mashabiki wa Argentina , lakini kwetu sisi mambo yalikuwa tofauti kwa sababu sote tunapenda soka.''

Mashabiki wengi mjini Rio walichagua Copacabana kama sehemu ya kukutana na kutazamia michuano hiyo.

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Alejandro Yemes ni raia wa Venezuela na Danielle Voellinger ni mmarekani

Alejandro Yemes raia wa Venezuela na Danielle Voellinger mmarekani walikutania Vila Madalena.

"tulikutanahishwa na rafiki yetu, ambaye sote wawili tunamjua kwani tulisoma naye karibu na mji wa Sao Paulo na tukakubaliana kukutana katika kombe la dunia,'' asema Alejandro.

'Mitandao ya mapenzi'

Uhusinao wa kimapenzi pia umenawiri kwenye mitandao, kwa usaidizi wa programu za mapenzi au 'Apps'.

Moja ya programu hizo ni Tinder, ambayo ilishuhudia ongezeko la kutumiwa wakati wa kombe la dunia.

Valentina mwenye umri wa miaka 33 anasema amekuwa akitumia programu hiyo wakati huu kutafuta mapenzi.

"kwangu mimi , sio tu kuwa na uhusiano wa mapenzi na watu, mimi hupenda kuwasaidia wageni wanapofika Brazil. ''

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Douglas Rodriguez

Hadi sasa amekutana na watu wawili, mmoja kutoka Uswizi na mwengine mmarekani.

Programu za mapenzi pia zimekuwa zikitumiwa na watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja. Programu ya mapenzi inayotumiwa na wapenzi wa jinsia moja 'Grindir' ilipata ongezeko la asilimia 31 ya watumiaji wakati huu wa kombe la dunia.

Hili halijanishangaza, kuna wachezaji wengi ambao wamejitangaza kushiriki mapenzi ya jinsia moja.Kwa hivyo iwe mchezaji au shabiki, wote wanatumia programu hiyo. ''

Douglas Rodriguez,mwenye umri wa miaka 22 kutoka Porto Alegre, anasema kuwa tangu kuanza kutumia programu hiyo wakati huu wa mashindano, amekuwa akienda kurusha roho zaidi ya mara tatu kwa wiki na watalii ambao amekutana nao kwenye mtandao.