Riek Machar asema hana uchu wa madaraka

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Riek Machar anasema kuwa wananchi wanapigania uhuru wao

Aliyekuwa makamu wa Rais Nchini Sudan Kusini,Daktari Riek Machar, anasema kuwa anachozungumzia kwa sasa ni kutafuta sera ya mfumo mpya wa uongozi wa taifa hilo inayokabiliana na mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Machar kwa sasa anaongoza vita vya upinzani dhidi ya serikali ya Rais Kiir. Anasema kuwa anapigania mageuzi wala sio kutaka wadhifa katika utawala wa sasa.

Riek Machar ameiambia BBC kuwa mfumo huo unastahili kufaidi kila mtu Nchini humo na kuonyesha kuwa nchi hiyo ina demokrasia

Mwezi uliopita serikia na waasi walikubalina kuunda seriali ya umoja wa kitafa katika kipindi cha siku sitini.

Lakini baada ya kuulizwa ikiwa hilo litafanyika bwana Machar alikataa kujibu.

Sudan Kusini ilipata uhuru miaka mitatu iliyipita lakini mwaka uliopita ilitumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii