Marekani yatafuta mwafaka Afghanistan

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wafuasi wa mgombea wa urais nchini Afghanistan Abdullah Abdullah

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry anaanza awamu ya pili ya mazungumzo nchini Afghanistan hii leo katika juhudi zake za kutaka makubaliano kuhusu matokeo ya raundi ya pili ya uchaguzi wa urais.

Bwana Kerry anatarajiwa kukutana na wagombea wawili Ashraf Ghani na Abdullah Abdullah.

Afisa mmoja mwandamizi nchini Marekani anasema kwa sasa mazungumzo hayo yanaangazia maswala mawili ikiwemo uchunguzi kuhusu madai ya udanganyifu na kuimarisha mazungumzo ya kisiasa kati ya wagombea hao wawili.

Afisa huyo amesema kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa serikali mpya ya Afghanistan inashirikisha kila mmoja.