Israel yaendeleza mashambulizi yake Gaza

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mashambulizi ya Israel katika eneo la Gaza

Mashambulizi ya angani yemeendelea kutekelezwa katika eneo la Gaza usiku kucha huku Israel ikijaribu kulizuia kundi la wapiganaji wa Hamas kurusha mamia ya makombora katika maeneo ya Israel.

Maafisa wa Palestina wanasema kuwa zaidi ya watu 120 wameuawa tangu mashambulizi hayo yaanze.

Umoja wa mataifa unasema kuwa wengi wao ni raia wa kipalestina.

Palestina inasema kuwa vijana wawili walemavu nchini humo wameuawa baada ya shambulizi moja la angani kupiga jumba moja lililokuwa likitumiwa na masharika ya hisani katika mji wa Beit lahiya.

Mashambulizi ya roketi kutoka Gaza yameendelea huku ving'ora vya mashambulizi ya angani vikisikika katika maeneo mawili kusini mwa Israel.

Mazungumzo yanaendelea katika umoja umoja wa mataifa ili kutafuta suluhu ya kusitisha vita hivyo.