HRW:Serikali ya Iraq iliwauwa wafungwa

Image caption Shirika la kutetea haki za binaadamu, Human Rights watch

Shirika la haki za binaadamu,Human Wrights Watch linasema kuwa vikosi vya serikali ya Iraq pamoja na wanamgambo vinadaiwa kuwauawa zaidi ya wafungwa 250 wakati vikosi hivyo vilipokuwa vikitoroka mashambulizi ya wanamgambo wa ISIS mwezi uliopita.

Human Wrights watch linasema kuwa lina rekodi ya kile ilichokitaja kuwa mauaji ya halaiki katika miji na vijiji sita tofauti.

Shirika hilo lenye makao yake mjini New York nchini Marekani limesema kuwa mauaji hayo yanaonekana kuwa ya kulipiza kisasi kufuatia mashambulizi ya wanamgambo wa kisunni.

Wafungwa wote waliouawa ni watu wa dhehebu la kisunni huku idadi kuu ya wanajeshi wa Iraq wakiwa watu wa dhehebu la kishia.

Shirika la Human Rights Watch limesema kuwa mauaji ya wafungwa ni ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.