Ashtakiwa kwa kuvizia siri za Marekani

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ndege za kivita za Marekani

Mamlaka nchini Marekani imemshtaki mfanyibiashara mmoja raia wa Uchina kwa kudukua mifumo ya kompyuta za kampuni kadhaa ili kuiba habari kuhusu miradi ya kijeshi.

Akishirikiana na watu wengine wawili ,Su Bin anatuhumiwa kwa kuingilia data za kampuni zilizo na kandarasi za ulinzi ikiwemo Boeing kati ya mwaka 2009 na 2013.

Nakala za mahakamani zinaonyesha kuwa mshtakiwa alikuwa anatafuta habari za ndege mbili za kivita pamoja na ndege moja ya kubeba mizigo ya kijeshi ili kujaribu kuyauzia makampuni ya serikali ya Uchina.

Bwana Su alikamatwa nchini Canada mnamo mwezi Juni.

Hatahivyo hakutoa tamko lolote kuhusu madai hayo.